Duka lisilo na muuzaji lafunguliwa Tokyo

Muktasari:

  • Duka hilo lina kamera takriban 80 kwenye paa na rafu za kuwekea bidhaa zilizounganishwa na mfumo wa AI unaobainisha bidhaa zilizochaguliwa na mteja.


Tokyo, Japan. Duka lisilosimamiwa na binadamu linalotumia teknolojia ya AI badala ya muuzaji, lilitarajiwa kuanza kufanya kazi Jumatano kwa majaribio kwenye kituo cha treni jijini Tokyo.
Shirika la Reli la JR East, limepanga kufungua duka hilo Jumatano kwenye kituo chake cha Akabane Kaskazini mwa jiji la Tokyo.
Wateja wataweza kutumia kadi zao za kielektroniki zilizotolewa na makampuni ya usafirishaji, kuingia na kufanya manunuzi kwenye maduka hayo.
Duka hilo lina kamera takriban 80 kwenye paa na rafu za kuwekea bidhaa zilizounganishwa na mfumo wa AI unaobainisha bidhaa zilizochaguliwa na mteja.
Mfumo wa maduka yasiyo na muuzaji tayari umekwishaanza kutumika kwenye baadhi ya maduka nchini China. Kampuni kubwa ya uuzaji bidhaa mtandaoni ya Marekani, Amazon, imefungua maduka ya aina hiyo huko Seattle.