Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kenya hatarini kuporwa mali zake

Muktasari:

  • Mikasa ya mali za nchi kuchukuliwa imeshuhudiwa kabla ikiwa katika nchi ya Tajikistan, ambako China ilipatiwa ardhi ili iweze kupunguziwa deni lake.

Nairobi, Kenya. Ripoti ya kampuni ya utafiti kimataifa iliyotolewa na Taasisi ya Huduma ya Uwekezaji ya Moody’s imeiweka Kenya miongoni mwa nchi zilizoko kwenye hatari kubwa ya mali zake kuchukuliwa na wakopeshaji China kutokana na deni kubwa.
Taasisi ya Moody's inasema kwamba Kenya iko katika hatari ya kupoteza udhibiti wa miundombinu muhimu ya kimkakati kama bandari na reli ambayo iko katika majadiliano na China.
Kampuni hiyo ya utafiti imesema kwamba China ama haitoi majibu linganifu au haiko wazi katika kufafanua mataifa ya Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo yanakabiliwa na shinikizo la kufilisiwa.
Mikasa ya mali za nchi kuchukuliwa imeshuhudiwa kabla ikiwa katika nchi ya Tajikistan, ambako China ilipatiwa ardhi ili iweze kupunguziwa deni lake.
Mataifa mengine, kwa mujibu wa Moody’s, yaliyoko kwenye hatari ya mali za kimkakati kuchukuliwa na China ni Angola, Zambia na DR Congo, ambayo yote ni tajiri kwa rasilimali asilia.
Kwa mujibu wa Hazina, hadi kufikia mwishoni mwa Septemba, deni ambalo Kenya ilikuwa inadaiwa na China lilifikia dola za Marekani 5.4 bilioni (Shilingi za Kenya 554.88 bilioni) au asilimia 73.4 ya deni lote linalofikia Sh756.28 bilioni (dola 7.3 bilioni), ambalo kwa kiasi kikubwa linahusishwa na ujenzi wa reli ya kisasa.