Kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi Tanzania; Mti mmoja kwa wakati

Muktasari:

  • Mradi wa Kilimanjaro (TKP) ni mradi wa kijamii na kimazingira unaolenga kuondoa madhara ya mabadiliko ya tabianchi katika mkoa wa Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla.

“Fikiria kama kila Mtanzania angepanda mti mmoja kila mwaka, tutafikia uwezekano wa kupanda miti zaidi ya milioni 50 kila mwaka.” – Rais mstaafu, Benjamin Mkapa.

TKP ni nani na wanafanya nini?

Mradi wa Kilimanjaro (TKP) ni mradi wa kijamii na kimazingira unaolenga kuondoa madhara ya mabadiliko ya tabianchi katika mkoa wa Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla.

Malengo yao ni kupanda mamilioni ya miti kila mwaka ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuinua maisha ya watu wanaoishi karibu na mlima. Wanalenga kutafuta majawabu ambayo yanaleta faida za kiuchumi kutunza miti badala ya kuikata.

Msisitizo wao ni katika manufaa ya kimazingira na kiuchumi. Kwa kutambua hilo, Mradi wa Kilimanjaro siyo tu unahamasisha utambuzi wa mabadiliko ya tabianchi bali pia uhitaji wa hatua za haraka, siyo tu Kilimanjaro bali Tanzania na ulimwenguni kote.

Aprili – Disemba 2018 ulikuwa msimu wao wa kwanza wa upandaji miti. Mpaka kufikia mwisho wa mwaka, watapanda miti 100,000. Hata hivyo, katika kampeni zao mbalimbali wanalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kupanda miti milioni moja kabla mwaka 2019 haujaisha.

Jitihada zao siyo katika upandaji miti pekee, bali wanafuatilia pia miti inayopandwa kwa ushirikiano na Greenstand kupitia App yao, kuhakikisha kwamba miti inaishi na kuendelea kukua. Wanazishirikisha jamii, shule na kuzihamasisha kuunga mkono jitihada za kupanda m

Miti inayopandwa ina asili ya Tanzania, hivyo inaweza kustahimili mazingira ya mahali inapopandwa. Baadhi ya miti iliyopandwa kwenye maeneo ya jamii na shule ni miti ya matunda ambayo inaongeza manufaa kwa wanafunzi na watu wanaoishi kwenye jamii husika.

TKP wanafurahia hatua waliyofikia mpaka sasa; wakidhamiria kuongeza kiwango mwaka 2019. Washirika wao ni mashirika na makampuni binafsi ambayo yanachangia muda na rasilimali fedha, huduma za kujitolea na kampeni za uhamasishaji.

Unawezaje kusaidia?

Mradi wa Kilimanjaro unamwalika kila mtu aliyepo Tanzania kuungana nao katika jitihada. Jiunge nao na changia mti kupitia jukwaa la mtandaoni au M-Pesa na kuwa sehemu ya mabadiliko. Pia, kuna zawadi za kujishindia kila wikendi.

Fuata hatua hizi rahisi hapa