Mchungaji Msigwa atolewa nje bungeni

Walinzi wa bunge wakimuondoa Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msingwa ndani ya ukumbi wa bunge kwa kukaidi kiti cha Naibu spika Tulia Akson, wakati wabunge wakichangia hoja ya kumpogeza Rais John Magufuli kwa kuwezesha ununuzi wa korosho za wakulima, jijini Dodoma leo. Picha na Ericky Boniphace

Muktasari:

Naibu Spika amemtoa nje ya Bunge, mbunge Peter Msigwa kwa alichodai kuwa mbunge huyo wa Iringa Mjini alikuwa akipiga kelele

Dodoma. Naibu Spika Dk Tulia Akson amemtoa nje Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa wakati Bunge likichangia Azimio la kumpongeza Rais kuhusu uamuzi wa Serikali kununua korosho za wakulima.

Uamuzi wa Naibu Spika umefuatia mabishano baina yake na Mchungaji Msigwa baada ya kumtaja Mbunge huyo kuwa alikuwa anapiga kelele.

Dk Tulia alimuonya zaidi ya mara tano kumtaka Msigwa akae chini lakini Mbunge huyo aligoma ndipo akamtaka atoke nje na alipogoma aliwaita askari wamtoe nje na wakatekeleza.