RC Mnyeti: Manyara iko pazuri uanzishaji viwanda 100

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti amesema mkoa wake unaendelea vizuri na utekelezaji wa agizo la Waziri wa Tamisemi Seleiman Jafo la kuhakikisha kila mkoa unaanzisha viwanda 100.

Hanang. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti amesema mkoa wake umetekeleza agizo la Waziri wa Tamisemi Suleiman Jafo la kuhakikisha kila mkoa unaanzisha viwanda 100.

Mnyeti amesema hayo leo Novemba 18 wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Samia Suluhu wilayani Hanang ambapo amesema hadi Septemba 30 mwaka huu kulikuwa na viwanda vipya 29, 25 vimekarabatiwa na vinafanya kazi, tisa ujenzi wake unaendelea na sita ujenzi haujaanza.

Amesema wana matarajio kuwa Manyara itafikia malengo yake na kuyavuka ya viwanda vipya zaidi ya 100 kabla ya Desemba mwaka huu aa ofisi yake inaendelea kuhamasisha wananchi kuwekeza katika viwanda ili kukuza hali ya uchumi ya mkoa na Taifa kwa ujumla.

"Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2013 za ofisi ya takwimu ya Taifa zinaonyesha kuwa mkoa wa Manyara una viwanda 2,400 kati ya hivyo viwanda vidogo sana ni 2,067 vidogo 305, vya kati 14 na vikubwa ni 14," amesema Mnyeti.