Video: Kivuko cha Mv Nyerere chaanza kunyanyuliwa

Muktasari:

Kazi ya kukinyanyua kivuko cha Mv Nyerere kilichopinduka Septemba 20 imeanza ambapo sehemu kubwa ya chini ya kivuko hicho imeanza kuonekana tofauti na awali. Kazi hiyo inafanywa na wataalam wa uokoaji kutoka JWTZ wakishirikiana na wenzao wa Songoro Marines

Ukara. Wataalam wa uokoaji kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na wenzao wa kampuni ya Songoro Marines ya jijini Mwanza wameanza kukinyanyua kivuko cha Mv Nyerere.

Tayari sehemu kubwa ya chini ya kivuko hicho kilichopinduka Alhamisi iliyopita ya Septemba 20, 2018 kimeanza kuonekana tofauti na awali.

Kazi ya kukinyanyua kivuko cha Mv Nyerere inafanyika baada ya wataalam hao wakishirikiana na wazamiaji kufanikiwa kupenyeza mipira maalum (maboya) kujazwa upepo.

Kwa mujibu wa mtaalam kutoka Songoro Marines, Major Songoro, maboya hayo yako saba na kila moja lina uwezo wa kunyanyua tani 18.