Kiwanda cha sukari cha Magereza kuzalisha tani 30, 000 kwa mwaka

Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (mwenye miwani) na ujumbe wake wakiwasili Gereza Mbigiri Mkoani Morogoro jana tayari kwa kukagua eneo la uwekezaji wa Kilimo cha Miwa na Uzalishaji wa Sukari. Picha kwa hisani ya michuzi blog

Muktasari:

Jeshi la Magereza limefufua kiwanda hicho na shamba la miwa la Gereza la Mbigiri mkoani Morogoro.

Dar es Salaam. Kiwanda cha sukari cha Jeshi la Magereza kilichokuwa kimefungwa mwaka 1996 kinatarajia kuzalisha tani 30, 000 kwa mwaka baada ya kuanza tena uzalishaji.

Jeshi la Magereza limefufua kiwanda hicho na shamba la miwa la Gereza la Mbigiri mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati Magereza wakisaini mkataba wa makubaliano na mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF, kupitia Kampuni Tanzu ya Mkulazi Limited, Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema kazi  ya ukaguzi na ya kitaalamu imeshafanyika na tani 30,000 za sukari  zitazalishwa kwa mwaka.