Kongamano la biashara kati ya Ufaransa na Tanzania lazinduliwa

Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu

Muktasari:

  • Ameitaka jumuiya ya wafanyabiashara nchini kutumia fursa zinazoweza kupatikana katika kongamano hilo kukuza uchumi.

Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu amezindua kongamano la biashara baina ya Ufaransa na Tanzania.

Ameitaka jumuiya ya wafanyabiashara nchini kutumia fursa zinazoweza kupatikana katika kongamano hilo kukuza uchumi.

"Kila mtu katika dunia ya leo anafahamu umuhimu wa sekta binafsi kwenye uchumi wa nchi. Serikali inaendelea kuweka mazingira sawa ili kurahisisha uwekezaji," alisema Makamu wa Rais.