Lissu ashinda kwa kishindo TLS

Arusha. Mwanasheria Tundu Lissu ameshinda kwa asilimia 88 ya kura zote baada ya kupata kura 1411 kati ya 1682 zilizopigwa katika uchaguzi huo.

 Zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa Tanganyika Law Society (TLS) lilikamilika leo saa tano asubuhi.

Upigaji kura ulianza saa 12:00asubuhi ambapo mawakili walipiga kura kwa kupanga mstari na kuchovya kidole kwenye wino.

Hadi zoezi hilo lilipokamilika majira ya saa 5:15 hakuna vurugu zozote zilizotokea na mawakili wengi wamejitokeza tofauti na chaguzi zote zilizowahi kufanyika.

Tunaendelea kusubiri taarifa rasmi  za matokeo ya uchaguzi huo.