Lissu asomewa mashtaka ya uchochezi

Muktasari:

  • Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) anadaiwa kutoa maneno yaliyokuwa na lengo ya kuleta chuki dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amefikishwa katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashtaka  ya kutoa lugha ya uchochezi.

Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri  leo Jumatatu, Julai 24, mahakama imeelezwa kuwa Lissu ametoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali Julai 17 akiwa maeneo ya Ufipa, Kinondoni.

Imedaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo ya kuleta chuki dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alipotakiwa kukubali ama kukataa  makosa hayo na Hakimu Mashauri, Lissu amesema kusema kweli haijawahi kuwa kosa  la jinai.

Kwa sasa upande wa mashtaka wameomba Lissu anyimwe dhamana na upande wa utetezi wanapinga hoja ambazo bado zinaendelea.