Lukuvi ahimiza matumizi ya mashine za matofali nafuu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akipata maelezo ya ujenzi nafuu alipotembelea banda la maonyesho la NHC jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya makazi duniani. Picha na Salim Shao

Muktasari:

  • Akizungumza jana, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi  amesema mashine hizo ni za kutengeneza matofali yasiyotumia saruji nyingi na akawataka wananchi kutumia teknolojia hiyo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.

Dar es Salaam. Wakati Tanzania ikiadhimisha siku ya makazi duniani leo imeelezwa kuwa , Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) ulitengeneza mashine  80 za kufyatulia matofali kwa mwaka 2015/16.

Akizungumza jana, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi  amesema mashine hizo ni za kutengeneza matofali yasiyotumia saruji nyingi na akawataka wananchi kutumia teknolojia hiyo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.

Amesema wakati wa ujenzi, matofali hayo ya kufungamana huunganishwa bila kutumia saruji na hivyo kupunguza gharama za ujenzi.

Lukuvi alisema wakala hiyo inaendelea kutoa mafunzo ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ambapo vikundi 110 vimeshanufaika kwenye wilaya za Kahama, Morogoro na Kinondoni.

mwisho
Siku ya makazi duniani huadhimishwa siku ya Jumatatu ya mwanzo wa mwezi Oktoba kila mwaka.