Maalim Seif afanya kikao maalum Unguja

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif

Muktasari:

Juzi, Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi juzi aliandika barua inayomtambua Profesa Lipumba kuwa Mwenyekiti wa chama hicho hali iliyowakusanya wafuasi wake kukusanyika katika ofisi za chama hicho Buguruni na baadaye mwanasiasa huyo kuingia katika ofisi yake.

Wakati Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akijiandaa kuzungumza  na wafuasi wake leo  jijini hapa, Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif naye yupo kwenye kikao maalum kinachoendelea hivi sasa Vuga, Unguja.

Juzi, Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi juzi aliandika barua inayomtambua Profesa Lipumba kuwa Mwenyekiti wa chama hicho hali iliyowakusanya wafuasi wake  katika ofisi za chama hicho Buguruni na baadaye mwanasiasa huyo kuingia katika ofisi yake.

 Mwandishi wetu aliyeko eneo la tukio sasa hivi anaendelea kutujuza yanayojiri.

Kwa taarifa hii zaidi na nyingine nyingi  nunua gazeti lako la Mwananchi kesho au soma mtandaoni BONYEZA HAPA