Maalim Seif ajipa matumaini

Muktasari:

Tangu kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, 2015, Maalim Seif amekuwa akitoa kauli za matumaini akisema: “Mambo yaelekea kuwa mazuri.”

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad bado anaamini atakuwa Rais wa Zanzibar akidai kwamba nchi alizopeleka malalamiko yake zimefikia katika hatua nzuri.

Tangu kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, 2015, Maalim Seif amekuwa akitoa kauli za matumaini akisema: “Mambo yaelekea kuwa mazuri.”

Hata hivyo, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aliyeshinda katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20, 2016 ambao Maalim Seif aligoma kushiriki, amekuwa akisema kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kumwondoa madarakani, awe wa ndani au nje ya nchi.

Akizungumza katika kipindi cha Funguka kinachoendeshwa na Tido Mhando kupitia Kituo cha Televisheni cha Azam, Maalim Seif alisema wananchi wasifikiri kuwa mataifa hayo yamenyamaza, bali suala hilo litapatiwa ufumbuzi na atapata haki yake hivi karibuni.

Habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi