Madiwani wa CUF Tanga mikononi mwa Maalim Seif

Muktasari:

Akizungumza ofisini kwake juzi, Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe  alisema madiwani hao na mbunge watajadiliwa na mkutano mkuu utakaoongozwa na Maalim Seif, utakaoamua hatima ya mgogoro huo.

Tanga. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amealikwa kuhudhuria mkutano mkuu wa Oktoba 29, utakaowajadili madiwani wa chama hicho  kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga waliopigana kwenye kikao cha kamati ya utendaji.

Akizungumza ofisini kwake juzi, Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe  alisema madiwani hao na mbunge watajadiliwa na mkutano mkuu utakaoongozwa na Maalim Seif, utakaoamua hatima ya mgogoro huo.

 Jumbe alisema mkutano huo utakuwa na ajenda mbili; hatima ya mgogoro wa umeya wa Jiji la Tanga na nidhamu ambayo itawahusu madiwani 11 na Mbunge wa Tanga Mjini, Mussa Mbaruk.