Madiwani wamfutia hati ya umiliki shamba mwenyekiti CCM Monduli

Picha ya Mtandao

Muktasari:

  • Maamuzi hayo yametangazwa leo na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Isack Copriano na kueleza tayari baraza hilo limekwishatoa maagizo kuondolewa wavamizi hao.

Monduli. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Monduli mkoani Arusha wamefuta hati za mashamba matatu yaliyo ndani ya msitu wa Lendikinya likiwamo shamba la Mwenyekiti wa CCM, wilaya hiyo, Loota Sanare. 

Maamuzi hayo yametangazwa leo na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Isack Copriano na kueleza tayari baraza hilo limekwishatoa maagizo kuondolewa wavamizi hao.

Hata hivyo, Sanare akizungumza na Mwananchi leo amekiri kumiliki shamba ndani msitu ila akadai kuna shinikizo la kumuondoa ni la kisiasa.

"Nimesikia wanasema waniondoe mbona kuna wamiliki wengine wameachwa na pia mimi tayari niliwashinda Mahakamani,"alisema