Tuesday, February 13, 2018

Majaliwa ataja maeneo zinakopitishwa dawa za kulevya

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) akimkabidhi gari Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Sianga leo katika viwanja vya Karimjee,  jijini Dar es Salaam. 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imebaini maeneo ya bahari kuu, bandari, vituo vya mabasi na viwanja vya ndege ndio yanatumika zaidi kupitisha dawa za kulevya.

Amesema wafanyabiashara, wasambazaji na watumiaji wa dawa hizo wameendelea kukamatwa lengo likiwa ni kuhakikisha biashara hiyo inamalizika nchini.

Taarifa iliyotolewa leo Februari 13, 2018 na ofisi ya Waziri Mkuu imesema kuwa kiongozi huyo ametoa kauli hiyo wakati akikabidhi gari kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupamban