Maghembe aifumua misitu, wanyamapori

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe .

Muktasari:

Katika mabadiliko hayo, Maghembe amewabadilisha uongozi na vituo vya kazi maofisa watatu, huku wafanyakazi 43 wa kada nyingine kutoka wizarani humo wakihamishwa vituo  vya awali na kupangiwa maeneo mengine.

Dodoma. Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ameifumua idara ya misitu na wanyamapori, huku akimtangaza Robert Mande kuwa Kaimu Mkurugenzi  wa Uzuiaji Ujangili.

Katika mabadiliko hayo, Maghembe amewabadilisha uongozi na vituo vya kazi maofisa watatu, huku wafanyakazi 43 wa kada nyingine kutoka wizarani humo wakihamishwa vituo  vya awali na kupangiwa maeneo mengine.

Profesa Maghembe amefanya mabadiliko hayo zikiwa zimepita siku nne tangu alipoagizwa kufanya hivyo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kufanya ziara idara ya misitu.

Majaliwa aliagiza idara hiyo kufumuliwa na kusukwa upya kwa madai inalalamikiwa zaidi.