Magufuli amteua Kamanga kuongoza NIC

Samwel Peter Kamanga ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Muktasari:

  • Taarifa ia Ikulu imesema leo kuwa Kamanga aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo ameteuliwa kushika wadhifa huo kuanzia leo Oktoba 27, 2016.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Samwel Peter Kamanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Taarifa ia Ikulu imesema leo kuwa Kamanga aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo ameteuliwa kushika wadhifa huo kuanzia leo Oktoba 27, 2016.