Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Magufuli atishia kubadili noti kuwabana wanaoficha fedha

Rais Magufuli atishia kubadili fedha

Muktasari:

Akizungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo mchana mjini hapa, Magufuli amesisitiza kuwa kauli hiyo ni mahsusi kwa watu walioficha fedha katika majumba yao na kuwataka kuachana na tabia hiyo mara moja ili fedha hizo ziingie katika mzunguko.

Dar es Salaam. Katika kile kinachoonekana kutaka kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha, Rais John Magufuli amesema kwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua kubadili fedha ili zile zinazofichwa na watu hao wakose mahali pa kuzipeleka.

Akizungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo mchana mjini hapa, Magufuli amesisitiza kuwa kauli hiyo ni mahsusi kwa watu walioficha fedha katika majumba yao na kuwataka kuachana na tabia hiyo mara moja ili fedha hizo ziingie katika mzunguko.

Huku akisisitiza kuwa katika utawala wake fedha za bure hazitakuwepo kwa sababu zilizokuwepo awali zilitokana na fedha za wizi kutoka serikalini ambazo kwa sasa zimedhibitiwa, alisema kwa mwendo anaokwenda nao sasa ni ngumu kwa mwananchi kupata fedha bila kufanya kazi.