Mahanga amwangukia Msemakweli

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Maendeleo ya Vijana, katika Serikali ya Awamu ya Nne, Makongoro Mahanga

Muktasari:

  • Hata hivyo Msemakweli amesema hawezi kumsamehe Mahanga kutokana na kwamba ameshatumia gharama katika kesi yake hivyo lazima alipwe fedha zake.

 

  • Mahanga anatakiwa kumlipa Msemakweli jumla ya Sh11, 097,000 na anatakiwa kulipa Sh2 milioni kila mwezi kwenye akaunti ya
  • Msemakweli na kisha kuwasilisha mahakamani risiti ya malipo, hadi deni hilo litakapomalizika.

Dar es Salaam. Katika hali inayoonyesha hali ngumu ya kiuchumi, aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Maendeleo ya Vijana, katika Serikali ya Awamu ya Nne, Makongoro Mahanga ameamua kujisalimisha na kumwangukia Kainerugaba Msemakweli ili amsamehe deni analomdai.

Hata hivyo Msemakweli amesema hawezi kumsamehe Mahanga kutokana na kwamba ameshatumia gharama katika kesi yake hivyo lazima alipwe fedha zake.

Mahanga anatakiwa kumlipa Msemakweli jumla ya Sh11, 097,000 na anatakiwa kulipa Sh2 milioni kila mwezi kwenye akaunti ya

Msemakweli na kisha kuwasilisha mahakamani risiti ya malipo, hadi deni hilo litakapomalizika.

Deni hilo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli katika kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa na Mahanga dhidi yake baada ya kumtaja katika kitabu chake cha Orodha ya Mafisadi Sugu wa Elimu kuwa ni mmoja wa vigogo wenye shahada za Udaktari wa Falsafa za kughushi.