Majaliwa: Serikali imeshalipa madeni ya Sh29 bilioni

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Muktasari:

  • Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imelipa jumla ya Sh29 bilioni  kwa watumishi mbalimbali wa umma wakiwemo walimu ikiwa ni sehemu ya madeni yao.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imelipa jumla ya Sh29 bilioni  kwa watumishi mbalimbali wa umma wakiwemo walimu ikiwa ni sehemu ya madeni yao.

Majaliwa amesema hayo wakati wa uzinduzi wa vyumba vitatu vya kisasa vya madarasa katika shule ya sekondari Iwawa iliyoko wilayani Makete.

Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kumaliza madeni ya watumishi hao, ambapo hadi kufikia Novemba mwaka jana kiasi hicho cha fedha kililipwa kwa watumishi 31,000.