Majaliwa awahakikishia mikopo wanafunzi elimu ya juu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa kilele cha maadhimsho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Picha na Ofisi ya Wiziri Mkuu

Muktasari:

Majaliwa alisema hayo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia kesho, asilimia 90 ya wanafunzi watakuwa wameshapata fedha zao za mkopo wa elimu ya juu.

Majaliwa alisema hayo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

 “Serikali haitavumilia tena ucheleweshwaji wa makusudi wa malipo ya fedha za mikopo ya chuo. Kama kuna tatizo, taarifa zitolewe haraka ili kuzuia migogoro kati ya wanafunzi na Serikali yao,” alisema.

Habari Zinazohusiana