Rose Muhando; kondoo aliyetengwa na wachungaji

Miaka ya 2000 mwanzoni. Natoka Moro kurudi Dar. Kilichonipeleka huko ni shoo ya Joseph Mbilinyi ‘Sugu’. Akiwaaga mashabiki wa Moro baada ya kutangaza kuachana na muziki. Kwa kile alichodai kutaka kujikita kwenye biashara. Uamuzi huu ulishitua watu.

Kwenye ubora wake analisusa game? Watu hawakuamini. Daslama yote ilidondoka Moro. Ndani ya ukumbi wa Mango Park. Kila ukigeuka unakutana na sura za watoto wa Kino, Sinza, Ilala. ‘Masista Duu kwa Mabrazameni’ waliiteka Moro usiku mzima.

Hakuacha muziki kwa mapenzi yake kabla ya kurejea tena kwa kishindo. Kulikuwa na mazingira ya chuki kwa wadau wakubwa wa muziki wakati ule dhidi yake. Ndo maana hakutaka kuondoka bila kuaga watu aliokaa nao muda mrefu (mashabiki). Chuki zinaua sanaa.

Vurugu za usiku ule. Mitungi mingi na hofu ya vijana kulala peke yao. Kulipokucha tulikuwa hoi kwa uchovu. Baada ya supu tu, urafiki na udongo mwekundu wa Moro ulikufa. Safari ya kurejea Dar ikaanza nikiwa na Kebby na Jerry. Kawaida safarini watu hutekwa na ngoma za dini.

Hii safari ilinipa nafasi nzuri ya kumfahamu dada mwenye sauti ya pekee. Pumzi na mizuka ya kutangaza neno la Mungu kwa nyimbo. Nilimsikiliza kuanzia Mikese mpaka Ubungo. Nikamuelewa na nikahusudu uwezo wa Rose Muhando.

Kuanzia hapo si mimi tu. Wabongo wakamuelewa. Wakampenda. Mpaka nje ya mipaka yetu. Kimbiza sana waimbaji wenzake kwa shoo. Wingi wa mashabiki na mauzo ya albamu. Kila tamasha hakukosa. Msama anamuachaje Rose?

Rose wa sasa si yule tena. Kawa yeyote. Thamani yake inabaki kwenye ubinadamu kama binadamu. Ule ubora uliofanya waumini na viongozi wa dini mbalimbali kumlilia akatangaze neno kwa nyimbo kwenye mimbari zao. Umetoweka.

Binadamu ufanyacho leo ni kwa ajili ya kesho yako. Ingawa hakuna ajuaye kesho. Ndo maana ya hujafa hujaumbika. Siku ukiwa peke yako umelala ardhini ukizungukwa na udongo pande zote. Ukizikwa ndiyo maana halisi ya ulivyoumbwa.

Mama wa watoto watatu. Muda mrefu alilalamikiwa kupokea pesa bila kutokea kwenye matamasha. Mwanzo ilionekana anachafuliwa na wanahabari.

Muda hauna urafiki na kiumbe chochote. Yametimia. Majaribu yanakuja wakati ambao viongozi wa dini hawako tayari tena. Kumtafuta, kumweka chini na kumlea kiroho. Kumtia moyo na ujasiri arudi kama awali. Kaachwa bila msaada.

Neno linasema ni yupi (mchungaji) ambaye akipoteza kondoo mmoja katika

mia anaowachunga, hatawaacha wale tisini na tisa mahali salama na kutoka kwenda kumtafuta mmoja aliyepotea? Wachungaji wa leo wanamuacha kondoo na dunia yake.

Wamekomaa na wale kondoo 99. Rose

kaachwa. Ukristo unafundisha upendo ambao ulimvuta Rose kutoka imani nyingine na kujiunga nao. Pia tunaambiwa samehe unapokosewa. Kosa lake ni lipi lisilosameheka? Tumeamua kuhukumu?

Anaharibikiwa waimbaji wenzake wakimuangalia kama sinema. Ama pengine ni nafuu kwao kusikika. Ndo maana huoni wakifanya jambo kwa ajili yake. Anasemwa kwa mabaya tu. Tunaaminishwa hawezi kuwa mwadilifu tena.

Wiki hii imesambaa video ikionyesha anaombewa na mchungaji mmoja ambaye bila kutegemea akili ya CIA unagundua anatafuta ‘kiki’ tu. Rose kageuzwa kituko mpaka katika nyumba za ibada huku watu wanatazama kama Shilawadu. Inaumiza.

Haya mambo yapo kwa jamii yote. Thamani ya mtu ni pale anapokuwa na kitu. Mioyo yetu imejenga himaya ya roho chafu ya kutopenda kuona mwingine akifanikiwa. Kwenye tasnia ya muziki wa kidunia na kiroho ndo kambi rasmi ya ubinafsi na chuki. Hawapendani.

Katika wakati huu hutakiwi kushangaa kauli ya Fid Q. Kwa umri wake sidhani kama alitumwa. Na kama ni yeye mwenyewe atakuwa wa ajabu akisema hakumaanisha vile ambavyo wengi waliamini juu ya kauli yake. Mtu mzima huchutama kisha hukausha yapite.

Katika tangazo la wasanii kwa shoo ya Fiesta inayofanyika leo hapa Dar. Fid alitamka maneno ambayo yalitafsirika kama dongo kwa Wasafi na Festival yao. Kwamba “wanaanza wao (Fiesta) kisha wapumbavu wanaiga (Wasafi).” Fid alikoga mvua ya mitusi ya mashabiki wa WCB.

Sikushangaa. ‘Team’ za mitandaoni matusi ni sehemu ya maisha yao kama ibada kwao. Kilichoniacha hoi ni maneno ya Babu Tale na Mkubwa Fella.

Nikadhani ‘trend’ za mitandao kuvuta mashabiki lakini kutukanana mpaka kwenye uumbaji wa Mungu, ilivuka mipaka. Kuna maisha nje ya shoo za Fiesta na Wasafi Festival ambayo hawa jamaa watahitajiana. Fid alichotaka alipata kutoka kwa watoto wa kiswahili.

Unaweza kutafakari inauma kiasi gani kuona watu wanakushambulia kwa maradhi uliyonayo mwilini. Tena ni maradhi ya kudumu ambayo huwezi kupona. Zaidi, ni maradhi ambayo hukupata katika harakati za duniani. Isipokuwa ulizaliwa nayo.

Hizi chuki kwenye biashara ya muziki! Ni chanzo cha kuzalisha kiumbe kingine hiki ambacho ni tofauti na Rose Muhando tuliyemfahamu miaka yote. Hizi chuki ndo zinamuacha Rose adhalilike, atukanwe, achoreshwe na wachungaji bila msaada.

Tusitengeneze kina Rose wengine, niwakumbushe Fella na Tale, mafanikio ni zaidi ya kumiliki gari. Msiwaaminishe watoto wanaotaka kuwa kama Ya Moto Band, Temba au Chegge, Tunda Man au Keisha waamini mafanikio ya muziki ni kumiliki ndinga.

Alichofanya Fid Q ni kilekile kilichofanywa na wengi 2011 akiwemo Fella na Tale, wakati huo wakiwa ‘pro’ Clouds. Vinega wa Ant Virus walipoandaa shoo pale Chuo cha Ustawi wa Jamii. Kauli za watu kama Fiq juu ya Vinega zilikuwa nyingi wakidhani masela watafeli.

Kilichofanywa na Vinega ndicho anafanya Diamond. Tofauti ni kwamba Diamond ana wadhamini. Ila matusi ni yaleyale kama ya Vinega kuanzia mitandaoni mpaka kwenye nyimbo. Wanaficha kidogo tu. Fid anatukanwa kama alivyotukanwa Fella na Vinega.

Kwa maana hiyo Vinega wangeungwa mkono vya kutosha wakati ule. Leo tusingesikia malalamiko ya wasanii. Wote wanaowaunga mkono Wasafi Festival wakiponda Fiesta, ndiyo waliowaponda Vinega na kuwaunga mkono Clouds. Maisha ya dunia hii pacha wake ni unafiki.

Wasafi Festival ni ongezeko la ajira kwa vijana. Fursa zinapanuliwa. Wanamuziki wako wengi haiwezekani wote kupanda jukwaa la Fiesta. Nawakumbusha tu kuwa wasanii waliolala ‘geto’ ni wengi kuliko waliopo kwenye shoo hizo. Acheni chuki.

Watanzania tupo milioni 55. Ukileta bidhaa nzuri utapata walaji wa kutosha. Fiesta na Wasafi wanajenga nyumba moja ya muziki. Acheni kugombea fito. Narudia tena “Robo tatu ya wanamuziki nchi hii wanatazama hizi shoo kama mashabiki.” Hawajapata nafasi.

Tunataka Fiesta na Wasafi Festival za kutosha.

Leo Jumamosi hapa Dar es Salaam kuna sikukuu ya kitaifa kubwa moja tu. Ukidondoka Jiji la Korosho Mtwara nenda Nangwanda Sijaona. Tafuna korosho kisha Jibebe. Konki

Wimbo haufai ni kweli. Lakini usihalalishe kuupinga kwa kigezo kuwa siwezi kuusikiliza mbele ya wazazi. Kwa sababu hata vipindi vya redio na runinga ni vingi ambavyo siwezi kusikiliza na kutazama mbele ya wazazi. Lugha inayotumika ni ya kipuuzi tu. Lakini jamii ya sasa ndo inataka.

Watangazaji wanajisifia kwa ulevi kwenye vipindi vyao naanzaje kusikiliza mbele ya mzazi? Kuna mengi yanatendeka ambayo siwezi kutazama au kusikiliza si tu mbele ya wazazi bali hata mbele ya wadogo zangu, kuliko huo wimbo wa WCB.

Tupo kwenye dunia ya vita ya maadili.

Sitaki kuhalalisha kuwa wimbo hauna tatizo. Hapana, mimi natatizwa na adhabu iliyotolewa. Kwani wimbo ukiachwa YouTube kuna tatizo gani? Kule ndiko zipo nyimbo chafu zaidi ya hiyo. Sasa utawazuiaje watoto wasiharibiwe na hizo zingine ila ya Rayvanny na Diamond tu?

Basata wamekataza wimbo usichezwe mpaka jukwaani. Shoo nyingi zinafanyika usiku watoto wataharibiwa vipi muda ambao wamelala majumbani? Hivi maneno yale ni hatari kuliko matukio ya kishenzi yanayofanywa na mashabiki kwenye shoo za usiku? Shoo nyingi usiku hutawaliwa na uzinzi.

Dunia inaenda kasi ikiwaacha wazee nyuma mno. Badala ya kupinga kinachofanywa na vijana wa dunia ya sasa. Ni vyema tukawashika mkono wazee wetu. Mwana FA waambie wazee hao, kuwa dunia ya sasa inamuhitaji zaidi Haminamuhitaji zaidi Hamisa Mobetto kuliko Mchungaji Mama Rwakatare. Lazima tukubali kwamba upepo wa mambo yaliyokuwa ya kijinga siku za nyuma umekuwa mkali sana. Unatusukuma na kutupeleka unakotaka wenyewe na sisi tunaenda kama maboya.

Rostam na “Kibamia”, unadhani wehu? Weusi na “Unanifanya nicum”, ulifikiri hawana akili? Na “Iokote”, ya Maua Sama? Alipitiwa na shetani? “Aibu” ya Nandy ni kichaa? “Katika” ya Navy Kenzo? Hizi nyimbo zote si kwamba watu hawaelewi kinachomaanishwa. Jamii inajua na ndiyo mambo inayoyataka.

Vipi kuhusu “Jibebe” na “Kwangaru” za Wasafi? Utasema hawajielewi? Na unayesema hawajielewi huna lolote zaidi ya kumhifadhi msichana wa kazi “beki tatu” na mshahara wa masimango kibao. Hao unaosema hawajielewi wameajiri mamia ya watu mitaani. Wanafanya jamii inachotaka.

Wimbo haufai ni kweli. Lakini usihalalishe kuupinga kwa kigezo kuwa siwezi kuusikiliza mbele ya wazazi. Kwa sababu hata vipindi vya redio na runinga ni vingi ambavyo siwezi kusikiliza na kutazama mbele ya wazazi. Lugha inayotumika ni ya kipuuzi tu. Lakini jamii ya sasa ndo inataka.

Watangazaji wanajisifia kwa ulevi kwenye vipindi vyao naanzaje kusikiliza mbele ya mzazi? Kuna mengi yanatendeka ambayo siwezi kutazama au kusikiliza si tu mbele ya wazazi bali hata mbele ya wadogo zangu, kuliko huo wimbo wa WCB.

Tupo kwenye dunia ya vita ya maadili.

Sitaki kuhalalisha kuwa wimbo hauna tatizo. Hapana, mimi natatizwa na adhabu iliyotolewa. Kwani wimbo ukiachwa YouTube kuna tatizo gani? Kule ndiko zipo nyimbo chafu zaidi ya hiyo. Sasa utawazuiaje watoto wasiharibiwe na hizo zingine ila ya Rayvanny na Diamond tu?

Basata wamekataza wimbo usichezwe mpaka jukwaani. Shoo nyingi zinafanyika usiku watoto wataharibiwa vipi muda ambao wamelala majumbani? Hivi maneno yale ni hatari kuliko matukio ya kishenzi yanayofanywa na mashabiki kwenye shoo za usiku? Shoo nyingi usiku hutawaliwa na uzinzi.

Dunia inaenda kasi ikiwaacha wazee nyuma mno. Badala ya kupinga kinachofanywa na vijana wa dunia ya sasa. Ni vyema tukawashika mkono wazee wetu. Mwana FA waambie wazee hao, kuwa dunia ya sasa inamuhitaji zaidi Hamihitaji zaidi Hamisa Mobetto kuliko Mama Rwakatare. Ni vita ya maadili.