Sababu za vijana kushindwa kutengeneza mtandao wa ajira

Muktasari:

  • Unahitaji watu ili uweze kupata taarifa zitakazokusaidia kuajiriwa. Unafanyaje kujenga imani na watu hawa? Makala haya yanakusaidia kuelewa baadhi ya makosa yanayoweza kukufanya usiaminiwe na watu unaowahitaji.

Ujenzi wa mtandao wa watu unaoaminiana nao ni mtaji muhimu katika ajira. Ingawa ni muhimu kuwa na ujuzi na uzoefu katika eneo lako la umahiri, bado mafanikio yako kwenye soko la ajira yanategemea uimara na aina ya mtandao wa watu wanaokuamini. Huu unaitwa mtaji jamii.

Ingawa si mara zote, lakini kuna ukweli kuwa aina ya watu unaofahamiana nao inaweza kuamua aina ya ajira utakayopata. Kuna kada ya watu usipofahamiana nao, utapitwa na taarifa muhimu zisizotangazwa hadharani. Taarifa hizi zingekusaidia kupata ajira au kukuza ajira uliyonayo.

Unapotafuta ajira, kwa mfano, ni muhimu kuelewa kuwa mara nyingi waajiri hutafuta mtu anayeaminika kupitia vyanzo vinavyoaminika. Ukitegemea kupata taarifa za kazi kupitia matangazo rasmi, unaweza kujikuta ukitupwa nje ya ushindani wa soko.

Hapa ndiko uliko umuhimu wa kijana anayeingia kwenye soko la ajira kujifunza namna ya kutengeneza na kudumisha mitandao ya ajira. Mtandao wa ajira, kimsingi, ni mawasiliano ya karibu anayokuwa nayo mtafuta kazi au mwajiriwa na watu wenye uzoefu na ujuzi zaidi yake kwa lengo la kumsaidia kukua kiujuzi.

Katika makala haya, tunaangazia sababu nne kubwa zinazowakwamisha vijana kutengeneza mtandao madhubuti wa ajira.

Kupuuza watu unaofahamiana nao

Kama kijana una watu unaofahamiana nao tayari. Kuna watu uliosoma nao, waumini wenzako, marafiki wa ndugu zako, majirani na watu wengine unaokutana nao bila kutarajia. Watu hawa ni mtaji wako wa kwanza katika safari yako ya kutengeneza mtandao wa watu mnaoaminiana.

Bahati mbaya, na mara nyingi kwa kutokuelewa, vijana wengi wanafikiri watasaidiwa na watu wenye majina makubwa katika jamii. Wanatumia nguvu nyingi kutafuta imani na watu wapya lakini wakishindwa kuaminika na watu ambao tayari wanafahamiana nao.

Utashangaa maisha yako kazini yanakuwa mepesi kila siku. Unaweza kustaajabu bosi ambaye kila mtu anamwogopa kwa ukali na usumbufu mwingine, akija kwako mnazungumza kwa upendo na kuheshimiana.

Hivyo, jiheshimu, heshimu viongozi pamoja na wafanyakazi wenzako. Hakikisha uvaaji wako ni mzuri wenye kuendana na mazingira ya kazi yako, kisha uchape kazi kuzidi kiwango ambacho watu wangekitarajia kutoka kwako.

Unapaswa kuwa mtu mwenye malengo. Jiwekee malengo ya kazi na uyafikie. Njia hiyo itakufanya uonekane mtu bora zaidi kazini na utamvutia mwajiri kila siku.

Kuwa sehemu ya wafanyakazi

Ukiingia kazini, usitake kujionyesha kuwa wewe ni jeshi la mtu mmoja. Ni kweli unatakiwa uzingatie zaidi kile ambacho kimekufanya uajiriwe, lakini hapo kazini kuna wafanyakazi wenzako ambao kwa namna moja au nyingine utahitaji ushirikiano wao.

Unaweza kujiona unajtosheleza kikazi, kwa hiyo ukaona huhitaji kuuliza wala kumshirikisha yeyote kile unachofanya, lakini wewe ni binadamu. Unaweza kuumwa ghafla kazini na wafanyakazi wenzako ndiyo watakaotakiwa kukupa msaada.

Hivyo, ukiingia kazini jambo la kwanza hakikisha unafahamiana na wafanyakazi wenzako. Hakikisha unajuana nao majina, na umwite unayemhitaji kwa jina lake. Ni kosa kumaliza wiki nzima kazini ukiwa hujachukua hatua yoyote kujua majina ya wafanyakazi wenzako.

Ukiwa mgeni kazini, hakikisha kila siku katika siku zako za mwanzo, uwe unatumia angalau dakika 20 kuzungumza na wafanyakazi wenzako japo wawili, mbadilishane uzoefu kuhusu kazi. Upate kile ambacho wamekuwa wakifanya kila siku, nawe utoe ulichonacho.

Mazungumzo na wafanyakazi wenzako, yatakusaidia kujua mwajiri wako anapenda nini na mambo gani hapendi. Utakachokipata kitakusaidia kujitengenezea njia za kuishi ukiwa kazini.

Hakikisha mahudhurio mazuri

Siku za mwanzo ingia kazini mapema na ujitahidi kutoka kazini ukiwa umechelewa. Baada ya hapo, hakikisha hiyo ndiyo inakuwa tabia yako siku zote.

Ukiwa mpya kazini epuka visingizio na maombi ya ruhusa ya hapa na pale. Onyesha