Makamba awajia juu waliovamia misitu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba akizungumza na wakazi wa  Kata ya Kibindu wilayani Bagamoyo juu ya uvamizi uliofanywa na wakazi hao katika msitu wa  hifadhi wa  Zigua.

Muktasari:

  • Makamba ametoa msimamo huo leo alipotembelea msitu huo uliopo Kata ya Kibindu katika Halmshauri ya Mji Mdogo wa Chalinze mkoa wa Pwani kisha kuzungumza na wananchi wa eneo kwenye mkutano wa hadhara.
  • Amesisitiza kuwa wananchi hao waliovamia lazima waondoke katika eneo hilo ili kuhifadhi na kuulinda msitu Ziguo ambao ni miongoni vyanzo vya maji katika mto Wami.

Bagamoyo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema  Serikali itawaondoa na kuwashtaki mahakamani wananchi waliovamia na kuweka makazi katika hifadhi ya msitu Zigua kinyume cha sheria.

Makamba ametoa msimamo huo leo alipotembelea msitu huo uliopo Kata ya Kibindu katika Halmshauri ya Mji Mdogo wa Chalinze mkoa wa Pwani kisha kuzungumza na wananchi wa eneo kwenye mkutano wa hadhara.

Amesisitiza kuwa wananchi hao waliovamia lazima waondoke katika eneo hilo ili kuhifadhi na kuulinda msitu Ziguo ambao ni miongoni vyanzo vya maji katika mto Wami.

"Eneo hili tutatumia sheria mbili za mazingira na misitu ambayo inasema mtu akiingia kwenye hifadhi ya msitu na kufanya shughuli za kibinadamu ni kosa la jinai na anaweza kufungwa."

"Naomba muwapelekee salamu wenzenu walioweka makazi waambie tutawashtaki na kuwapeleka mahakamani ili sheria ifaute mkondo wake," alisema Makamba.