Monday, March 20, 2017

Makonda ahutubia, asifu vita ya dawa za kulevya

 

By Peter Elias, Mwananchi pelias@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amehutubia wakati wa uzinduzi wa barabara za juu, Ubungo  na kujisifu kuwa  vita ya dawa za kulevya imesaidia vijana zaidi ya 11,000 kuacha matumizi ya dawa hizo.

 Makonda pia alisema amekabidhi miradi 20 ya maji Dawasco na kuwa miradi mingine itapunguza tatizo la maji kwa asilimia 90.

“Inawezekana kabisa asiwepo mtu anayekuunga mkono, lakini ipo siku Mungu atakuuliza Tanzania aliyokupa umeifanyia nini,”alisema Makonda na kupigiwa makofi

 Makonda alizungumza mara baada ya Rais John Magufuli, kuwasili Ubungo akiwa na gari la mwendokasi. Rais aliambatana na Rais wa Benki  ya Dunia, jim Yong Kim.  

 Rais Magufuli leo atazindua ujenzi wa barabara za juu, katika eneo hilo la Ubungo. 

-->