Makonda awazindua vijana Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Muktasari:

Akizungumza kwenye mahafali ya kidato cha nne ya  Sekondari ya St. Joseph Millenium, Makonda amesema vijana wanatakiwa kupanua mawazo yao kwa kufikiria kuanzisha miradi itakayowasaidia kuinua uchumi wao na taifa.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka vijana kuchangamkia fursa zilizopo nchini,  badala ya kulalamika.

Akizungumza kwenye mahafali ya kidato cha nne ya  Sekondari ya St. Joseph Millenium, Makonda amesema vijana wanatakiwa kupanua mawazo yao kwa kufikiria kuanzisha miradi itakayowasaidia kuinua uchumi wao na taifa.

Makonda amewataka vijana kuachana na dhana kuwa Serikali itawapa ajira, badala yake wabuni biashara na miradi.

“Vijana wengi hawataki kubuni kitu cha kuwainua kiuchumi. badala yake, wanataka kuajiriwa serikalini huku wakilalamika wamesahaulika, hiyo siyo kweli,” amesema.