Mambo yatakayotawala siku 30 Ukawa na CCM

Muktasari:

Hivi karibuni, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ilitangaza uchaguzi mdogo utakaofanyika Jimbo la Dimani, Zanzibar na wa madiwani katika kata 22 za halmashauri 21 za Tanzania Bara.

Dar es Salaam. Wanasiasa na wasomi wamesema hali ngumu ya maisha, Serikali kuzuia mikutano ya hadhara na ukosefu wa ajira ni baadhi ya hoja zitakazoibuliwa  kwenye kampeni zitakazoanza Desemba 23 hadi Januari 21, mwakani.

Hivi karibuni, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ilitangaza uchaguzi mdogo utakaofanyika Jimbo la Dimani, Zanzibar na wa madiwani katika kata 22 za halmashauri 21 za Tanzania Bara.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Nec, Ramadhani Kailima alitangaza uchaguzi huo utafanyika Januari 22, mwakani na kampeni zitatimua vumbi kuanzia Desemba 23 hadi Januari 21, 2017.

Serikali ilivipiga marufuku vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara badala yake iliruhusu ile ya ndani.

Habari kamili soma gazeti la Mwananchi