Manispaa ya Temeke yagawanywa

Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo

Muktasari:

Pia, kumefanyika mgawanyo wa madiwani wa kata husika,  wa viti maalumu na wabunge  kulingana na jiografia ya manispaa hizo mbili.

Dar es Salaam. Manispaa ya Temeke imebaki na kata 23 kati ya 31, zilizosalia zikienda kwa manispaa mpya ya Kigamboni baada ya kufanyika mgawanyo.

Pia, kumefanyika mgawanyo wa madiwani wa kata husika,  wa viti maalumu na wabunge  kulingana na jiografia ya manispaa hizo mbili.

Meya wa Temeke, Abdallah Chaurembo amesema manispaa hiyo inabaki na madiwani 31 wakiwamo wabunge wa majimbo ya Mbagala, Temeke na wa viti maalumu.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Nassib Mmbaga amesema baada ya kuvunjwa na kuzaliwa kwa Manispaa ya Kigamboni kutakuwa na uundaji wa kamati ambazo waliokuwa wajumbe wake wamehamishiwa Kigamboni.