Mapenzi yasababisha vifo vya baba na mwanaye

File Photo

Muktasari:

Mtumishi huyo wa Mungu, mkazi wa Kitongoji cha Elimu katika Kijiji cha Kaseme, Kata ya Kaseme wilayani hapa, Charles Mulima (55) amejinyonga  baada ya kumuua  binti yake Martha (15).

Geita. Mwijilisti wa kanisa la AICT amejinyonga kwa kamba ya katani baada ya kumuua binti yake aliyemtuhumu kuwa na uhusiano wa mapenzi.

Mtumishi huyo wa Mungu, mkazi wa Kitongoji cha Elimu katika Kijiji cha Kaseme, Kata ya Kaseme wilayani hapa, Charles Mulima (55) amejinyonga  baada ya kumuua  binti yake Martha (15).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo lilitokea Septemba 25, saa 12:00 jioni baada ya mwinjilisti huyo kumkuta binti yake akiwa na mwanaume, hivyo kuwatuhumu kuwa wana uhusiano wa mapenzi.

Mwabulambo amesema baada ya Mulima kumuadhibu mwanaye na kugundua amefariki dunia  alizunguka nyuma ya nyumba na kamba ya katani, kisha kujinyonga.