Marufuku kusambaza mafuta ya mashoga

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee  na Watoto, Ummy Mwalimu

Muktasari:

Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera baada ya kuzindua wodi ya wazazi, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee  na Watoto, Ummy Mwalimu amesema suala hilo halikubaliki na ni kukiuka miiko na maadili ya Watanzania.

Bukoba. Serikali imepiga marufuku miradi inayohusisha utoaji wa vilainishi kwa mashoga kama njia ya kukinga kundi hilo na maambukizi  ya Virusi vya Ukimwi (VVU).

Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera baada ya kuzindua wodi ya wazazi, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee  na Watoto, Ummy Mwalimu amesema suala hilo halikubaliki na ni kukiuka miiko na maadili ya Watanzania.

Amesema mashirika yasiyo ya Kiserikali yanaweza kutumia njia nyingine mbadala za kudhibiti maambukizi ya Ukimwi na siyo kutoa vilainishi ambavyo kwa upande wa pili vinaweza kuwa vinachochea tatizo hilo.

Awali, akizungumza katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, waziri huyo amesema kuwa Serikali iko mbioni kuandaa muswada wa sheria utakaowasilishwa bungeni ili kutunga sheria itakayomlazimisha kila mwananchi kuwa na bima ya afya.