Matumizi ya Sh5.8 bilioni za hisa kujadiliwa na wadau

Meya wa Jiji la Dar es Salaam,  Isaya Mwita

Muktasari:

Hisa hizo ni zile zilizotolewa na Kampuni ya Simon Group kama sehemu ya ununuzi asilimia 51 ya hisa za Uda.

Dar es Salaam.  Meya wa Jiji la Dar es Salaam,  Isaya Mwita amesema watakaa pamoja na wadau kujua cha kufanya kuhusu matumizi ya fedha Sh5.8 bilioni ambazo ni asilimia 51 ya hisa za Kampuni ya Uda.

Hisa hizo ni zile zilizotolewa na Kampuni ya Simon Group kama sehemu ya ununuzi asilimia 51 ya hisa za Uda.

 “Bado hatujafanya maamuzi, mwisho wa mwezi huu tutakuwa na majibu kuhusu fedha hizo na baraza (madiwani) lilisema tusizitumie fedha hizo, tukikaa na wadau mbalimbali tutajua cha kufanyia na taarifa tutawapa,” amesema Mwita.

Januari 25 mwaka huu Rais John Magufuli wakati akizindua mradi wa mabasi yaendayo haraka (Udart) alitoa siku tano kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kutoa maamuzi kuhusu matumizi ya fedha hizo.