Mbowe aitwa polisi, Lowassa azuiwa Dar

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Edward Lowassa (kulia)

Muktasari:

Katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji naye ameendelea kusisitiza msimamo wa chama chake wa kuitisha mikutano nchi nzima Septemba Mosi

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Rais John Magufuli na Chadema kutoa misimamo tofauti kuhusu kupigwa marufuku kwa mikutano ya kisiasa, Jeshi la Polisi limemuita Freeman Mbowe kwa mahojiano, huku hafla ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili ambayo Edward Lowassa angekuwa mgeni rasmi ikizuiwa.

Katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji naye ameendelea kusisitiza msimamo wa chama chake wa kuitisha mikutano nchi nzima Septemba Mosi, kauli aliyoitoa saa chache baada ya Rais Magufuli kusisitiza msimamo wa kuzuia maandamano na mikutano ya kisiasa isipokuwa kwa wale walioshinda kwenye udiwani na ubunge ambao watatakiwa kufanya hivyo kwenye maeneo yao tu.

 

Zaidi soma Gazeti letu la Mwananchi