Mbunge Sugu apata pigo

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi.

Mbeya. Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Chadema), amepata pigo baada ya mwenyekiti wa kampeni zake, Christopher Mwamsiku kufariki dunia akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Ikonda wilayani Makete, mkoani Njombe.

Sugu akizungumza kwa simu amesema kifo cha Mwamsiku ambaye pia alikuwa katibu wake ni pigo kwake na Chadema.

Amesema alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa takriban  miezi mitatu iliyopita.