Mbunge atumwa kwa mwekezaji

Muktasari:

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Dk Chegeni katika Uwanja wa Stendi ndogo wilayani hapa, wananchi walimtaka kushughulikia mgogoro huo kabla hawajavamia eneo hilo.

Busega. Wakazi wa Kijiji cha Sogesca, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, wamemtaka Mbunge wao, Dk Raphael Chegeni kumaliza mgogoro uliopo kati yao na mwekezaji, vinginevyo watamvamia kwa sababu hakufuata taratibu za ardhi.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Dk Chegeni katika Uwanja wa Stendi ndogo wilayani hapa, wananchi walimtaka kushughulikia mgogoro huo kabla hawajavamia eneo hilo.

“Awamu zinapita kila mbunge amekuwa akiahidi kuwa mmiliki wa eneo hilo ataondolewa kwa sababu hakufuata sheria kulichukua eneo hilo kutoka kwa makandarasi waliokuwa wakitengeneza barabara, ni lini sasa ataondoka katika eneo letu ?” alihoji Julius Mbofu.

Akijibu madai hayo, Dk Chegeni alisema utaratibu wa kumuondoa mwekezaji huo baada ya kufutiwa hati ya umiliki wa eneo hilo kwa  kukosa uhalali unaendelea. “Ukweli suala hili linatia aibu kwa Serikali yetu, haiwezekani raia wa kigeni kung’ang’ania eneo la kijiji,” alisema Dk Chegeni.