Mchimbaji mdogo auawa kwa mawe

Muktasari:

  • Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita.

Geita. Walinzi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) wanatuhumiwa kumpiga mawe na kumsababishia kifo, mchimbaji mdogo Chacha Galigi (30).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ameuagiza uongozi wa GGM kusafirisha mwili wa marehemu hadi Musoma na kugharamia mazishi.

Meneja Mawasiliano wa GGM, Tenga Bill amesema wamesikitishwa na tukio hilo.

Wakizungumzia tukio hilo, wachimbaji wadogo, Mahizo Kibule na Jackson Busia wamesema wanalazimika kuingia mgodini kutafuta riziki kutokana na ahadi ya Serikali ya kuwapa magwangala kutotimizwa.