Mchungaji Rwakatare akaribisha watanzania kuombea Taifa

Mchungaji wa kanisa la Assemblies of God, Getrude Rwakatare.

Muktasari:

  • Rwakatere amesema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari kuwa kongamano hilo linaitwa ‘Shilo’ ni la sita kuanzia Desemba  4-11 ambapo litafanyika katika kanisa hilo.
  • Ameongeza kuwa kwa mwaka huu jumla ya watu kutoka mikoa 24 watakusanyika kanisani hapo kwa siku nane kufanya maombi.

Dar es Salaam.  Mchungaji wa kanisa la Assemblies of God, Getrude Rwakatare amesema katika kuelekea mwaka mpya 2017 Watanzania mbalimbali wanakaribishwa katika kongamano la kufanya maombi ya kuombea Amani Taifa katika kanisa hilo.

Rwakatere amesema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari kuwa kongamano hilo linaitwa ‘Shilo’ ni la sita kuanzia Desemba  4-11 ambapo litafanyika katika kanisa hilo.

Ameongeza kuwa kwa mwaka huu jumla ya watu kutoka mikoa 24 watakusanyika kanisani hapo kwa siku nane kufanya maombi.

“Tutakayomuombea Rais, mawaziri na viongozi mbalimbali bila kusahau amani ya nchi ambayo ni tunu tuliyoachiwa na waasisi wa Taifa hili,” amesema Mchungaji Rwakatare.