Mgonjwa wa JPM aliyelazwa Muhimbili aruhusiwa

Muktasari:

Wambura aliungua mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa unachemka jikoni na mume wake katika Kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani mara.

Dar es Salaam. Neema Wambura (32), mgojwa aliyekuwa anatibiwa majeraha ya moto katika Hospitali ya Taifa Muhumbili (MNH) kwa udhamini wa Rais John Magufuli, ameruhusiwa baada ya kupona na sasa anaomba msaada wa mtaji wa biashara.

Wambura aliungua mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa unachemka jikoni na mume wake katika Kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani mara.

Kwa mara ya kwanza alitibiwa katika Hospitali ya MNH lakini mwezi uliopita Rais Magufuli aliagiza mama huyo arejeshwe hospital hapo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Jana akiwa katika wodi ya Sewahaji mara baaada ya kuruhusiwa, Wambura alisema yupo vizuri kuendelea na maisha ya kawaida ila matamanio yake ni kufungua biashara ya duka jijini Mwanza na hataki kurejea tena mkoani Mara.

Mkuu wa Idara ya upasuaji wa MNH, Dk Ibrahim Mkoma alisema kwa sasa mwanamke huyo ana uwezo wa kufanya kazi zote.