Sunday, February 18, 2018

Mgonjwa wa fistula atoroka hospitali

 

By Amina Juma, Mwananchi asangawe@mwananchi.co.tz

 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Dk Dennis Ngalomba amewataka wanawake wanaosumbuliwa na fistula kufika katika zahanati na vituo vya afya ili wafanyiwe utaratibu wa kusafirishwa kwa ajili ya matibabu katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.

Wito huo umekuja baada ya mwanamke aliyekuwa anasumbuliwa na fistula kutoroka katika Kituo cha Afya Gairo wakati akifanya taratibu za kumsafirisha kuelekea Dar es salaam. Dk Ngalomba alisema mgonjwa huyo alifika kituoni hapo mwezi huu na walipompima waligundua anasumbuliwa na fistula na ndipo walipomfahamisha kuwa anatakiwa kusafirishwa kwenda Dar es salaam.

Mratibu wa Uzazi Salama, Wilaya ya Gairo, Edifonsia Mhafigwa alisema wanawake wengi wamekuwa wakiamini zaidi tiba asilia kuliko za hospitali. “Wanakwenda kwenye tiba asilia japo wakati mwingine haziwasaidii,” alisema.

-->