‘Yanga hii ni hadi ubingwa msimu huu’

Beki wa kulia wa Yanga, Juma Abdul amesema baada ya kukaa kileleni kwenye msimamo wa ligi sasa hakuna kushuka mpaka ubingwa.

Muktasari:

  • Yanga inaongoza ligi ikiwana  pointi 46, pointi moja dhidi ya watani zao wa jadi, Simba (45), wakati Kagera Sugar inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 37.

Dar es Salaam. Beki wa kulia wa Yanga, Juma Abdul amesema  baada ya kukaa kileleni kwenye msimamo wa ligi sasa hakuna kushuka mpaka ubingwa.
Yanga inaongoza ligi ikiwana  pointi 46, pointi moja dhidi ya watani zao wa jadi, Simba (45), wakati Kagera Sugar inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 37.
Abdul alisema wamesota kwa muda mrefu kutafuta nafasi ya kukaa kileleni na sasa wamepata hivyo hawatakubali kushuka.
Alisema watahakikisha wanaipiga Stand Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ili waendelee kuongoza ligi na kuwatimulia vumbi wapinzani wao Simba.
“Tunajua ugumu wa ligi ulivyo katika mechi hizi za lala salama, lakini tumejipanga huku tukiwa na malengo tuliyojiweka kwamba ubingwa lazima utue Jangwani na hilo ndilo tutakalolifanya,” alisema Abdul.
Aliongeza: “Hakuna mechi rahisi, lakini mkiwa na malengo hakuna linaloshindikana hivyo wachezaji wote tumejipanga kuwa lazima tutetee ubingwa wetu na ndiyo maana kila wakati tunajituma ili kuhakikisha tunatimiza malengo yetu.
“Timu zote ni sawa kwenye ligi na zote tunaziheshimu, lakini  kwa sababu tunataka ubingwa, hakuna namna tutazifunga  zote ikiwemo na Simba na ubingwa tutachukua.”