Baada ya Ronaldo kunyoosha mikono kwa Real, Man United sasa yarudi upya kwa Morata

Muktasari:

  • Ronaldo anataka kuondoka Real kwa sababu klabu hiyo haijamuunga mkono katika kesi yake ya kudai kukwepa kodi kiasi cha pauni13milioni.
  • Lakini rais wa Florentino Perez ametuliza hali hiyo baada ya kutoka hadharani na kuunga mkono.

London, England. Manchester United imerudi upya kwa mshambuliaji Alvaro Morata, baada ya Cristiano Ronaldo kuonyesha yuko tayari kuendelea kubaki Real Madrid.

Ronaldo anataka kuondoka Real kwa sababu klabu hiyo haijamuunga mkono katika kesi yake ya kudai kukwepa kodi kiasi cha pauni13milioni.

Lakini rais wa Florentino Perez ametuliza hali hiyo baada ya kutoka hadharani na kuunga mkono.

Kwa uamuzi wa Ronaldo kubadili uamuzi, nafasi pekee kwa Man United kumsajili mshambuliaji wa Real, Morata.

Perez alisema: “Tunaimani na tunamwamini Cristiano kwa kuwa wakati wote amekuwa akifanya mambo yake kwa nia njema kwa sababu tunajua hivyo ndivyo alivyo.”

Sasa Man United itakuwa tayari kutoa pauni 60milioni kwa ajili ya kumsajili Morata (24), na inaaminika watakuwa wamemsainisha mkataba kabla ya kuanza kwa mazoezi ya mwanzo wa msimu huu Julai 9.