Beki wa Arsenal kutimkia Barcelona

Muktasari:

Mchezaji huyo mwenye miaka 22, mara kwa mara amekuwa akihusishwa kurejea katika dimba la Nou Camp licha ya kwamba ameongeza mkataba wake Novemba mwaka jana hadi 2023.

London, England. Beki wa Arsenal, Hector Bellerin amesema ni jambo la kipekee kusikia kwamba anatarajia kurudi klabu yake ya zamani ya Barcelona.
Mchezaji huyo mwenye miaka 22, mara kwa mara amekuwa akihusishwa kurejea katika dimba la Nou Camp licha ya kwamba ameongeza mkataba wake Novemba mwaka jana hadi 2023.
Awali, beki huyo tegemeo wa Arsenal mwishoni mwa mwaka jana alitoa ufafanuzi kuhusu kuhusishwa kuhamia klabu yake ya zamani ya Barcelona. Lakini badala ya kukanusha tarifa zilizoenea sasa huku kuhamia klabu hiyo amesema kwamba huenda tetesi hizo zikawa ni kweli.
Ni jambo zuri kwa sababu zimekuwapo klbau nyingi ambazo zinanihitaji la kati ya hizo nyingi mojawapo ni Barcelona ambayo ni kipenzi changu,” aliliambia gazeti la Sport.
Mchezaji huyo ambaye aliondoka Barcelona mwaka 2011 na kujiunga na Arsenal aliongeza kuwa, “Niliondoka Barcelona kwa sababu klabu ilikuwa hainiamini nikajiona kama mtu nisiye na thamani.”
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger wiki iliyopita alisema kwamba ilikuwa ni jambo gumu kuamini kwamba Bellerin anahitajika kusajiliwa na Barcelona wakati siyo muda mrefu umepita mchezaji huyo ameongeza mkataba wake kuendelea kuwapo hapa Uwanja wa Emirates.
Suala la Barcelona kuonyesha nia ya kumhitaji Bellerin inakuwa ngumu kulichukulia kwamba ni jambo la kweli,” aliwaambia waandishi wa habari na kuongeza kuwa, amesaini mkataba mpya na amebakiza miaka mingi ya kuitumikia klabu.

Bellirin ni miongoni mwa wachezaji ambao Barcelona inawawinda kwa ajili ya msimu ujao kwa ajili ya kuimarisha safu ya ulinzi, huku wakiwa kwenye mchakato wa kutafuta kocha ambaye atarithi mikoba ya Luis Enrique.
Mchezaji mwingine aliyepo kwenye rada za timu hiyo ni Srgi Roberto ambaye anatakiwa na klbauhiyo kwa ajili ya kuimarisha winga ya kushoto, huku Javier Mascherano naye akitakiwa kikosi hapo ili kuziba nafasi ya Alex Vida ambaye amekuwa majeruhi tangu Februari.
Pia wachezaji, Kyle Walker (Tottenham), Cedrid  Soares (Southampton) na Joao Cancelo wa Valencia  nao wanahusishwa kujiunga na miamba hao wa La Liga.