Bundi hajatoka Simba?

Muktasari:

  • Mara ya mwisho Simba kutwaa ubingwa ni msimu wa 2011/2012 na baada ya hapo hali imekuwa hali si hali ndani ya klabu hiyo kwa miaka minne iliyofuata na huu ukiwa wa tano.

Dar es Salaam. Nini kinaisumbua Simba?, kitu gani kimeipata timu hiyo ambayo ilikuwa ikitikisa kwenye Ligi Kuu bara misimu ya nyuma.

Mara ya mwisho Simba kutwaa ubingwa ni msimu wa 2011/2012 na baada ya hapo hali imekuwa hali si hali ndani ya klabu hiyo kwa miaka minne iliyofuata na huu ukiwa wa tano.

Mashabiki wa Simba wamekuwa wakisononeka kwa muda mrefu na hasa majina wanayopewa na watani zao Yanga yamekuwa mwiba mchungu ndani ya mioyo yao na wanatamani msimu huu Mungu aitendee muujiza klabu yao kwa kuwapa ubingwa ili iweze kutoka katika masimango wanayopata.

Hata hivyo, gazeti hili limebaini kuwa tatizo kubwa linaloisumbua klabu hiyo kwa miaka minne sasa ni kushindwa kutengeneza safu makini ya washambuliaji.