Dau la Pogba litavunjwa fasta

Muktasari:

Manchester United ilitawala vyombo vya habari wakati walipotoa euro 100 milioni kumsajili kiungo huyo  Mfaransa kutoka Juventus msimu huu.

Munich, Ujerumani. Oliver Kahn anaamini ni suala la muda tu kabla ya dau la uhamisho wa Paul Pogba wa euro100milioni  kuvunjwa na hofu yake kama Bayern Munich itaweza kushinda na klabu za England na Hispania endapo dau la usajili litapanda.

Manchester United ilitawala vyombo vya habari wakati walipotoa euro 100 milioni kumsajili kiungo huyo  Mfaransa kutoka Juventus msimu huu.
Kahn anaamini ni suala la muda tu kabla ya mchezaji kununuliwa kwa euro150milioni, japokuwa haamini kama Bayern wataweza kufikia dau hilo.
"Kiasi kikubwa cha fedha kitatumika katika vita ya kusaka saini ya wachezaji bora," Kahn alilimbia jarida la michezo la Ujerumani la Socrates.
"Nafikiri dau la euro150m sasa hivi litavunjwa. itakuwa ni changamoto kubwa kwa Bayern kusaini mchezaji wa kariba ya Franck Ribery na Arjen Robben katika siku za usoni.
"Swali kama Bayern atakuwa tayari kwenda katika njia hiyo wakati England na Hispania wenyewe wananunua nyota wake wa kiasi kikubwa cha fedha."
Javi Martinez bado ni mchezaji ghali wa Bayern aliyesajiliwa kwa euro 40m, japokuwa chipukizi wa Mreno Renato Sanches usajili wake mwisho utawaghalimu euro 80m kutokana na gharama za uhamisho huo.