England yapata pigo

Muktasari:

Jones anayechezea Manchester United alirudi klabuni hapo wakati wa mazoezi juzi  baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana matatizo ambayo hayakuwekwa wazi.

Majeruhi Phil Jones amejitoa kwenye kikosi cha England ambacho kimecheza mechi ya kirafiki na Ujerumani jana pamoja  mechi ya kufuzu kombe la dunia Jumapili.
Jones anayechezea Manchester United alirudi klabuni hapo wakati wa mazoezi juzi  baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana matatizo ambayo hayakuwekwa wazi.
Kutokana na taarifa hiyo kuchelewa kutolewa ilielezwa kwamba hakukuwapo mipango ya haraka ya kuwabadili kwa ajili ya mechi hiyo ya kirafiki ya ambayo ilitarajiwa kucheza jana kwenye Uwanja wa Signa Iduna Park.
Kocha wa timu hiyo alisema kwamba atamtazamia kwa ajili ya mechi ya Jumapili ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi  Lithuania na mchezaji wa Chelsea Gary Cahill hatacheza mpaka michezo ijayo.
Jones amecheza jumla ya michezo 22 katika mashindano yote ya Manchester United katika msimu huu, haTa hivyo anakabiriwa na majeraha kwenye goti na mguu jambo lililomfanya kushindwa kuingia uwanjani.
Kukosekana kwa mchezaji huyo huenda kukaathiri kikosi hicho cha England kutokana na umuhimu wake baada ya kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ilipokutana na Ufaransa mwaka Novemba 2015.