Sunday, November 20, 2016

Hat-trick ya Ronaldo yaiua Atletico MadridCristiano Ronaldo, Real Madrid

Cristiano Ronaldo, Real Madrid 

By Madrid, Hispania

Madrid, Hispania. Nyota Cristiano Ronaldo amerudi kwa kasi akifumania nyavu kwa kishindo, baada ya kufunga mabao matatu (hat trick) na kuiwezesha Real Madrid kuilaza Atletico Madrid kwa 3-0 katika uwanja wa Vicente Calderon kuamkia leo.

Kwa mantiki hiyo, Madrid imejiimarisha kileleni kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya mahasimu wao Barcelona, ambayo awali ililazimishwa sare ya bila kufungana na Malaga.

Zikiwa zimecheza michezo sawa, Real Madrid inaongoza baada ya kujikusanyia pointi 30, ikifuatiwa na Barcelona yenye alama 26 huku Atletico Madrid ikisalia na pointi 24.

Ronaldo alianza kutikisa nyavu katika dakika ya 23 baada ya kupiga mkwaju wa adhabu na kuwababatiza mabeki wa Atletico. Alizidi kuwapa furaha mashabiki wa Madrid baada ya kufunga kwa njia ya penalti dakika ya 71 kabla ya kukamilisha hat-trick katika dakika ya 77, baada ya kuunganisha krosi safi iliyopigwa na winga mwenye mbio, Gareth Bale.

-->