Mabondia Rashidi, Sayuni kuzichapa Nanenane

Muktasari:

Mwandaaji wa pambano hilo, Miraji Uliza amesema litakuwa la raundi 10 na litatanguliwa na mapambano mengine ya masumbwi kwa mabondia mbalimbali.

Dar es Salaam. Mabondia wa ngumi za kulipwa, Kais Rashidi na Faraji Sayuni watazipiga katika pambano la kuwania ubingwa wa Taifa wa kilo 57 Agosti 8 kwenye Ukumbi wa Kobelo Pub Manzese Dar es Salaam, ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wakulima ya Nanenane.

Mwandaaji wa pambano hilo, Miraji Uliza amesema litakuwa la raundi 10 na litatanguliwa na mapambano mengine ya masumbwi kwa mabondia mbalimbali.

Mapambano ya utangulizi yatakuwa kati ya Abdallah Pazi ambaye atazipiga na Said Mkone, Goodluck Mrema na Hassan Kiwale huku Omari Uliza akizipiga na Bruno Fadhili.

Wengine watakaopanda ulingoni ni Said Jelemi kumkabili Aziz Kondo na Saleh Mkalekwa akicheza na Salum Ngula, Aziz Uliza naye atapimana na Mohamed Matimbwa.