Man City yaifanyia umafia Man United

Muktasari:

Wakati mchezaji huyo alipokuwa amekata tiketi ya ndege kwenda Manchester Alhamisi usiku ilikuwa inafamikia kuwa alikuwa anakwenda Man  United.

Manchester, England. Kiungo Bernardo Silva amefanikisha uhamisho wake wa pauni 43milioni kwenda Manchester City akitokea Monaco na kuiacha solemb Manchester United.

Kiungo huyo mchezaji wa Ureno alikuwa akiwania zaidi na Jose Mourinho, lakini amebadili mwelekeo na kuamua kufanya kazi na Pep Guardiola.

Jose Mourinho alisema wiki hii kuwa anakiribia kumkaribisha Mreno mwenzake Old Trafford katika usajili wake wa msimu huu.

Wakati mchezaji huyo alipokuwa amekata tiketi ya ndege kwenda Manchester Alhamisi usiku ilikuwa inafamikia kuwa alikuwa anakwenda Man  United.

Kumbe alikwenda kutua katika City Football Academy na kusaini mkataba wake wa miaka mitano.

Aliwaambia viongozi wa City: “Ni faraja kubwa kuwa hapa, kuanzia sasa na mimi ni moja wa wachezaji waliokuwa katika timu bora duniani.

“Ninafuraha kuwa sehemu ya  timu ya Manchester City nitajitaidi kufanya kila niwezalo kutimiza malengo yangu na klabu pia.