Manahodha Mkude, Cannavaro wakaa benchi

Dar es Salaam. Kocha wa Simba, Joseph Omog  na mwenzake wa Yanga, George Lwandamina wameamua kuwake benchi manahodha wao Jonas Mkude na Nadir Haroub 'Cannavaro' katika mchezo huo wa watani wa jadi unaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kocha Simba, Mcameroon,  Omog alimwanzisha James Kotei na kumweka benchi Mkude katika mchezo huo katika vita yake ya kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Naye Mzambia Lwandamina alimrudisha kikosini beki wake Andrew Vicent 'Dante' aliyekuwa akitumikia adhabu ya kadi nyekundu na kumpumzisha Nadir 'Cannavaro'.

Cannavaro ni moja wa wachezaji wakongwe waliocheza mechi nyingi dhidi ya Simba tangu alipojiunga na mabingwa hao miaka 10 iliyopita.