Mashindano ya mbio yazinduliwa Moshi

Muktasari:

Akizindua mbio hizo jana, Warioba amewapongeza Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa mashindano hayo na wengine kwa kuyafanya kuwa makubwa ndani na nje ya nchi.

Moshi. Mashindano ya mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2017 yamezinduliwa mjini hapa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba.

Akizindua mbio hizo jana, Warioba amewapongeza Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa mashindano hayo na wengine kwa kuyafanya kuwa makubwa ndani na nje ya nchi.

“Mashindano haya pia yamechangia kukuza utalii kwani wanariadha wa kimataifa na wageni wao hufanya utalii baada ya mashindano na hivyo kufaidisha uchumi wa nchi,” amesema Warioba